/home/mhubiriw/public_html/kuokoka.php on line 24
" style="color:
Warning: Undefined array key "font" in /home/mhubiriw/public_html/kuokoka.php on line 25
">

Tafakari

Mhubiri wa Kimataifa



Mahubiri

Kuokoka

Ushauri

Maombi

Shuhuda

Maarifa



Kusudi la Injili ya Kimataifa

Changia Injili ya Kimataifa

Matangazo/Shukrani

Burudani za Injili

 

Kuokoka?

Kuokoka ni kuokolewa na Yesu ktk maisha dhambi na kurithishwa maisha ya haki ya yesu na baba yake kwa kupewa roho mtakatifu aliyebeba huo urithi wa mbinguni. Kuokoka kumetoka kwa Mungu aishiye mbinguni

Je unataka kuokoka?

Ukiwa umesoma mahubiri yetu ya injili ya kimataifa na uko tayari kuokoka yaani kutubu, kubatizwa na kujazwa roho mtakatifu kwa jina la yesu sema na ifuatishe sala ya toba inayombatana naa ukiri wa imani ya yesu na kumkaribisha roho mtakatifu kwa kumaanisha toka ndani ya moyo kuachana na dhambi na kumkaribisha yesu moyoni na ktk maisha yako atawale iliyopo hapo chini.

Sala ya kuokoka

Sema, "Bwana yesu ninakuja kwako mimi ni mwenye dhambi natubu naamini ya kwamba ulisulubiwa kwa ajili ya dhambi zangu na laana zake damu yako ilimwagika nipate ondoleo la dhambi na kupatanishwa na baba yako na ulipigwa nipate ondolewa dhambi zangu, nisamehe dhambi zangu na uniondolee bila kusahau laana zake na ulifufuka nipewe maisha mapya huru mbali na dhambi na laana zake yaani maisha ya haki na baraka Yesu ingia ktk maisha yangu na ufalme wa mungu pamoja na roho mtakatifu unipe maisha hayo ya haki yako na baraka zake pia.Andika jina langu mbinguni nijaze furaha yako ya kunisamehe na kuniondolea dhambi na laana yake na kufanyika mwana mbinguni na kupewa sehemu ya urithi wako wa kutembea na nguvu na mamlaka ya mungu wako ya kuzivunja na kuziharibu kazi za shetani ikiwepo mapepo,magonjwa n.k. Asante yesu kwa kuniokoa , kwa roho mtakatifu, kwa neema yako, kwa karama au vipawa vyako, mamlaka yako, ufalme wako na nuru yako maana umeyafanya maisha yangu kuwa na uzima wako ... Amen"

Hongera kwa Kuokoka: Ukiwa umesali sala hiyo ya kuokoka kwa kuamini toka ndani moyo umeokoka, leo siku ya kuzaliwa kwako kiroho kule mbinguni kama ulivyoingia duniani kwa kuzaliwa kimwili. Umekuwa mtoto mdogo kule mbinguni usiyefahamu mambo mengi yaliyomo ktk ufalme wa mungu kama ulivyozaliwa kimwili duniani ulipokuwa mdogo ulikuwa hujui dunia ilivyo hivyo kiroho kwa sasa huna ufahamu mkubwa juu ya ufalme wa mungu na mbinguni kwa baba yake yesu na amri za yesu za ufalme wa mungu unazopaswa kuzishika na kuzitenda ili maisha yako yapate kubadilika kuwa kama ya yesu alivyoishi duniani kwa kumpendeza mungu bila kutenda dhambi.

Form kwa waliokoka hasa watu wa kimataifa
Kama umeokoka kwa kukiri sala ya kuokoka hapo juu au kwa kwenda ktk huduma au kanisa la waliokoka au mikutano ya injili na kuokoka baada ya kusoma mahubiri ya injili ya kimataifa yaliyopo ktk tovuti hii na kuguswa na neema ya Baba yake Yesu wa mbinguni. Bofya --->>> Form kwa waliokoka hasa watu wa kimataifa

Sasa umeokoka unatakiwa ufanyeje?
Ukitaka kufahamu unachotakiwa kufanya bofya --->>> ushauri kwa aliyeokoka na kama una laana mfano ugonjwa kama uziwi, presha, kisukari,ugumba n.k au mapepo unahitaji maombi ili yaondolewe bofya --->>>maombi

Kitabu kidogo kwa waliokoka
Kitabu hiki ni kwa ajili ya kukupatia ufahamu kidogo juu ya kuokoka kile mungu amefanya ndani yako na maadiliko yanayotokea ndani yako baada ya kupata nguvu ya roho mtakatifu nguvu ya mungu usistaajabie unaweza kukisoma kwa kubofya --->>> Kitabu kidogo kwa waliokoka

                                                       Mark: 16: 14 - 18