/home/mhubiriw/public_html/lameck.php on line 23
" style="color:
Warning: Undefined array key "font" in /home/mhubiriw/public_html/lameck.php on line 24
">

Tafakari

Mhubiri wa Kimataifa



Mahubiri

Kuokoka

Ushauri

Maombi

Shuhuda

Maarifa



Kusudi la Injili ya Kimataifa

Changia Injili ya Kimataifa

Matangazo/Shukrani

Burudani za Injili


 

kuokoka
Mimi ni mtumishi wa mungu, mhubiri wa kimataifa lameck lister niliokoka mwaka 2003 nikiwa na umri wa miaka 17 kidato cha tatu ktk shule ya sekondari kibaha. Mtumishi wa mungu aliyetumiwa na Yesu kunihubiria Paulo Roberty kabla ya kuokoka aliitwa Everist Robert. Siku yangu ya kuokoka nilijazwa roho mtakatifu na kuongea kwa lugha mpya kama Yesu alivyosema ktk marko 16:16. Siku zote namshukuru Baba wa Bwana Yesu kwa kunijalia neema ya kuzaliwa mara ya pili mbinguni na kuwa mwana mbele zake. Kwa undani kuhusu mhubiri wa kimataifa Lameck Lister soma kitabu Mhubiri wa Kimataifa Book

Mafundisho ya kukulia wokovu
Mafundisho ya kukulia wokovu niliyapata ktk kanisa la Efatha mwaka 2003-2006. Yanahusu maisha mapya ya mtu aliyeokoka anavyotakiwa kuishi. Ndani ya hayo mafundisho yanazungumzia maisha ya toba. tofauti ya maisha kabla hujaokoka na baada ya kuokoka na kile Yesu na baba yake amefanya ndani ya mtu aliyeokoka.

Mafundisho ya Ubatizo wa maji mengi
Mafundisho ya ubatizo wa maji mengi niliyapata ktk kanisa la Efatha mwaka 2003-2006 nakubatizwa pia. Mafundisho ya ubatizo wa maji mengi kwa kifupi yanazungumzia kuzika utu wa kale pamoja na baraka ya kubadilisha jina baada ya kubatizwa. Maswali kama kwa nini ubatizwe kwa maji mengi wala si maji machache yana majibu ndani hayo mafundisho maana Yesu tunayemfuata ndivyo alivyobatizwa na mitume ndivyo walivyobatiza waaminio. kwa kuwa tunamfuata Yesu yatupasa kutimiliza haki yote kwa kufanana naye ktk ubatizo wa maji mengi.

Mafundisho ya Roho mtakatifu
Mafundisho ya roho mtakatifu niliyapata mwaka 2007 ktk kanisa la Efatha - Mwenge DSM Tanzania. Na kuwekewa mkono na Mtume na Nabii Josephat . E. Mwingira mkuu na mwanzilishi wa kanisa la Efatha ili kujaa roho mtakatifu kwa upya na vipawa au karama kama ilivyo neema ya Mitume itokayo kwa Yesu kristo.

Utumishi wa mungu
Baada ya kumaliza mafundisho yote nimepewa cheti cha utumishi wa mungu cha ufahamu wa cheo cha kristo. Natambulikana ndani ya kanisa la Efatha kama Mtumishishi wa mungu mbele baba yake Yesu na Yesu kama mhubiri wa kimataifa. Ukitaka kuona cheti cha utumishi wa mungu nilichopata Ktk Kanisa la Efatha
>>> bofya hapa

                                                       Mark: 16: 14 - 18