/home/mhubiriw/public_html/watumishi.php on line 23
" style="color:
Warning: Undefined array key "font" in /home/mhubiriw/public_html/watumishi.php on line 24
">

Habari njema

Tubuni

Ufalme wa yesu

Yesu na ufufuo

Yesu ndiye kristo

Mche mungu

Ubatizo wa maji mengi

Yesu ni bwana

Watumishi wa Yesu

 


"Baadaye akaonekana na wale kumi na mmoja walipokuwa wakila, akawakemea kwa kutokuamini kwao na ugumu wa mioyo yao, kwa kuwa hawakuwasadiki wale waliomwona alipofufuka katika wafu. Akawaambia, Enendeni ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe. ". (Marko 16:14-15)

Ni utaratibu wa mungu enyi wafanyakazi wakimataifa kutuma watumishi wake ili kusema na wanadamu aliowaumba tangu vizazi vya zamani hadi leo na hata vizazi vijavyo ndivyo atakavyosema navyo kwa kutuma watumishi wake . Utaratibu huu tunaupata kwa kusoma biblia yote jinsi mungu alivyoongea na watu wake kwa nyakati tofauti kwa kutumia watumishi wake aliowatuma je unaamini? kama unaamini sema Ameni.

Mungu aliwatumia manabii wake kama Musa, Yeremia na Isaya kusema na watu wake, kisha kwa nyakati zetu amemtumia Yesu , mitume kumi mbili kusema na watu wake na mwisho mtume Paulo ambaye alisema kwa habari ya mungu na kanisa kuendelea kutuma watumishi wake wa kusema wengine na kanisa na wengine na wanadamu ambao si kanisa na maneno ya roho mtakatifu kwa kinywa cha mtume Paulo aliyosema ni amina. Yesu ameweka ktk kanisa mitume, manabii , waalimu, wachumgaji na wainjilisti ambao anawatuma waseme na kanisa wengine waseme na watu ambao si kanisa hapa yupo mhubiri , mitume na washuhudiaji. hivyo mungu anaendelea na utaratibu wake wa kutuma watumishi hata leo kwa kanisa. wengine wanapaswa kuwasikiliza na kutendea kazi maneno ya mungu yanayosemwa na watumishi wa mungu waliotumwa naye tena huyathibitisha kwa ishara au huyatimiliza kwa miujiza.

Utawatambua watumishi waliotumwa na Yesu kwa matendo yao wanapotumiwa na mungu maana hufanana na Yesu kama yeye alivyotumiwa na mungu ktk kuhubiri, kufundisha, kutoa pepo,kuponya au kutenda miujiza. hivyo watumishi wa mungu waliotumwa na yesu hutumiwa kutenda mambo makuu kama hayo mungu aliyomtumia yesu kutenda ikiwemo, miujiza na ponyaji mbalimbali.Yako mengi ya kusema nawe ee mfanyakazi wa kimataifa ukiwa na kiu ya kuyafahamu okoka.

Yesu alikufa kwa ajili ya wenye dhambi na waovu apate kuwapatanisha na baba yake ambaye ndiye mungu aliyekuumba wewe mfanyakazi wa kimataifa. Hivyo anakuita upatane naye kwa kuamini yeye alikupenda sana wewe hata akamtoa mwanawe Yesu afe ili wewe upate kuokolewa kutoka ktk dhambi au maisha ya dhambi akupe maisha ya haki ya mwanaye yesu aliyeishi bila kutenda dhambi kwa kufanya mapenzi ya mungu yaani baba yake.

Ikiwa unaamini yesu alisulubiwa na kufa kwa ajili ya wenye dhambi wa kimataifa kama wewe wapate kuokoka na maisha ya dhambi maisha ya kunuka rushwa , ufisadi, matukano, wanawake wenye mitego, anasa za duniaa na umeamua leo kumgeukia yesu na kumfuata kwa kuachana na maisha ya dhambi na u tayari kupokea maisha ya uzima na haki ya yesu yaliyo huru mbali na dhambi na kuachana na ya kwako ya dhambi bofya Kuokoka

<<<|---kurudi nyuma

                                                       Mark: 16: 14 - 18